Soko la mbaazi bado hali ni tete


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Eng. Stella Manyanya amesema mbaazi ni chakula kizuri chenye protini na watanzania wanaweza kula badala ya kuwategemea watu wa maeneo mengine kununua
-
Amesema biashara ni ushindani na kila watu wanahakikisha wanakidhi soko lao la ndani, upande wa Tanzania wanaendelea kutafuta soko lakini wakati huo huo wanaendelea kusisitiza watu wapende kutumia mbaazi
-
Amesema Dodoma Mbaazi inauzwa mpaka 1,800 kwa kilo na soko la Dar es Salaam kwenye supermarket inauzwa mpaka 2,400 hivyo tusitegemee soko mpaka kutoka nje kwani hata ndani ya nchi bado kuna watu wanaweza kula
-
Amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye aliyeuliza "Serikali imefikia wapi kutafuta soko la Mbaazi baada ya msimu uliopita bei kushuka kutoka Tshs 2,000 mpaka 150?"
-
Nape amesema sasa ni msimu wa kilimo hicho, kama bado hali haieleweki wananchi washauriwe waachane na mbaazi na badala yake wajikite kwenye mazao mengine ambayo yana soko la uhakika

Comments